Home » , » MAKATIBU WA CCM WAPEWA PIKIPIKI NA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA ARUSHA

MAKATIBU WA CCM WAPEWA PIKIPIKI NA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA ARUSHA

Written By mahamoud on Friday, 3 July 2015 | 02:23

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki  Mh.Bernard Murunya amabye alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi pikipiki,akimkabidhi moja ya Pikipiki kwa katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha Rehema Mohamed jana katika makao makuu ya chama  hicho jijini Arusha, jumla ya pikipiki saba zilikabidhiwa kwa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha huku Mwenyekiti wa Taifa  Abdalah Bulembo pamoja Baraza kuu Taifa wakifanya jitihada za kupatikana kwa Pikipiki hizo,katikati ni Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi ambapo katika risala yake alisema kuwa ugawanyi wa pikipiki hizo saba ni juhudi za Mwenyekiti Taifa Abdalah Bulembo pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Taifa ,Tukio hilo ni la Jumuiya ya wazazi Nchi nzima la kuwakabidhi Makatibu wa Wilaya zote 161 pikipiki kwaajili ya kurahisisha utendaji wa kazi na kuboresha suala zima  la usafiri ikiwa ni kuimarisha Chama cha Jumuiya zote
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki  Mh.Bernard Murunya akijaribu moja ya pikipiki alizokabidhi
                        Makatibu wa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha wakiwa katika pikipiki zao
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akiwa anatoa maelekezo ya namna pikipiki hizo kutumika kwa uangalifu huku akiongeza kuwa endapo mtumishi atahamishwa kwenda sehemu nyingine basi atalazimika kuhama na pikipiki yake na akiweza kutunza vema baada ya miaka minne atazawadiwa kwa bei nafuu
Katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha mjini Rehema Mohamed akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa pikipiki jana jijini Arusha (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
Share this article :

Post a Comment




 
Support : Copyright © 2015. Habarika 24 Dev - All Rights Reserved
Customized by Bongotech