Home » , » FAINALI YA KOMBE LA COPA AMERICA 2015 CHILE VS ARGENTINA.

FAINALI YA KOMBE LA COPA AMERICA 2015 CHILE VS ARGENTINA.

Written By mahamoud on Friday, 3 July 2015 | 04:03

Fainali ya Kombe la Copa America 2015 tayari imepangwa baina ya wenyeji Chile dhidi ya Argentina ambao wanapewa kipaumbele kuibuka kidedea!

Fainali ya Kombe la Copa America 2015 tayari imepangwa baada ya Argentina kuwachapa Paraguay kipigo kitakatifu cha 6-1 kwenye mechi yao ya Nusu Fainali iliyochezwa Jumanne. Hatahivyo watacheza dhidi ya wenyeji wa mashindano, Chile ambao kwa sasa macho yao yote wameyaelekeza kwenye kombe hili na wanategemea kuwa wenyeji wa kwanza wa mashindano haya kushinda kombe hili tanguColombia ilipofanya hivyo mwaka 2001. 

Ingawa Paraguay waliweza kutoka nyuma kwa magoli 2-0 waliyofungwa na kisha kuweza kupata suluhu ya 2-2 dhidi ya Argentina kwenye mechi yao ya kwanza ya Ufunguzi, kamwe haikuwezekana kujirudia! Argentina waliwafunga Paraguay jumla ya magoli 6 katika namna ambayo ilijidhihirisha dhahiri kwamba uwezo wa kiwango chao hakika ulikuwa juu na tayari wamefuzu kuingia kwenye hatua ya Fainali ya Kombe la Copa America mara ya tatu kati ya mashindano 4 yaliyopita. Baada ya kufungwa mara mbili na Brazil mwaka 2004 na mwaka 2007, hakika watajituma kufa na kupona ili kudhihirisha ya kwamba wao ni bora! 

Wenyeji wa mashindano haya Chile wameweza kufika hatua ya Fainali kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo miaka 28 iliyopita na ni dhahiri vichwani mwao wana lengo moja tu ambalo ni – Ushindi! Baada ya kushindwa kupata kombe lolote kwenye mashindano katika historia ya taifa kutimiza miaka 99, na mwaka huu watacheza dhidi ya wapinzani wagumu sana fikiria uwepo wa – Lionel Messi,Angel Di MariaSergio Aguero na wababe Argentina! 

Kutakuwa na mechi ya kumtafuta mshindi wa nafasi ya 3 na 4, kwahiyo usikose kutazama mechi baina ya Peru na Paraguay mwisho wa wiki hii! 

Jumamosi, 04 Julai 2015
Share this article :

Post a Comment




 
Support : Copyright © 2015. Habarika 24 Dev - All Rights Reserved
Customized by Bongotech