Home » , » NI MSIBA TENA JAMBO CONCEPTS (T) LTD, WACHAPISHAJI WA GAZETI LA JAMBO LEO.

NI MSIBA TENA JAMBO CONCEPTS (T) LTD, WACHAPISHAJI WA GAZETI LA JAMBO LEO.

Written By mahamoud on Thursday, 2 July 2015 | 00:04

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Jambo Concepts (T) Ltd, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti na Jarida la Jambo Brand, limempoteza mfanyakazi wake mwingine wa idara ya masoko, Kinai Mtinda (pichani), baada ya kufariki dunia saa 7 usiku wa kuamukia leo katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach na taratibu zingine kuhusiana na msiba huo zitatolewa baadae.

Marehemu Kinai ameacha watoto wawili.

Kifo cha Mtinda kinakuja ikiwa ni siku chache tangu afariki dunia Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Ramadhani Kibanike mwishoni mwa mwezi uliopita. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe Amina.


Share this article :

Post a Comment




 
Support : Copyright © 2015. Habarika 24 Dev - All Rights Reserved
Customized by Bongotech