Home » , » MAHAKAMA KUU YAMUACHIA HURU SHEIKH PONDA.

MAHAKAMA KUU YAMUACHIA HURU SHEIKH PONDA.

Written By mahamoud on Thursday, 27 November 2014 | 20:50

Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.
MAHAKAMA  Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self  iliyokuwa inamkabili.
 
Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi,  Mkoani Morogoro inayomkabili.
(PICHA/HABARI : DEOGRATIUS MONGELA/GPL)
 Wakili wa Sheikh Ponda, Bw Juma Nassoro akizungumza jambo na mteja wake mahakamani hapo.
Sheikh Ponda  akitoka nje ya Mahakama Kuu baada ya kushinda Kesi ya Ardhi iliyokuwa ikimkabili kisha kurudi mahabusu katika gereza la Segerea.

 
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2015. Habarika 24 Dev - All Rights Reserved
Customized by Bongotech