Home » , » UWANJA WA NDEGE WA TRIPOLI WATEKWA

UWANJA WA NDEGE WA TRIPOLI WATEKWA

Written By mahamoud on Saturday, 23 August 2014 | 23:10

Uwanja wa ndege wa Tripoli.

Muungano mmoja wa wanamgambo nchini Libya unasema kuwa umeuteka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli baada ya mapigano makali kati yake na kundi pinzani la waasi.
Picha zilizowekwa katika mtandao zimeonyesha wapiganaji hao wakisherehekea juu ya ndege na katika majengo ya uwanja huo.
Muungano huo unaoshirikisha wanamgambo wa kiislamu pamoja na wanamgambo kutoka mji wa Misrata umesema kuwa uliuteka uwanja huo licha ya mashambulizi ya angani yanayodaiwa kutekelezwa na Misri pamoja na nchi za ufalme wa kiarabu.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema kuwa kuna ripoti za kuendelea kwa vita kati ya makundi pinzani viungani mwa mji huo.

Uwanja huo umefungwa kwa takriban mwezi mmoja sasa kufuatia vita kati ya makundi pinzani ya wanamgambo yaliozuka tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo kanali Gaddafi mwaka 2011. 
                                Source BBC Swahil.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2015. Habarika 24 Dev - All Rights Reserved
Customized by Bongotech